
Mjukuu wa Ibrahimu, Israeli alikuwa na wana 12. Taifa la kisasa la Israeli linaundwa na wana wawili tu kati ya hao – Yuda na Benyamini. Wana wengi wa Lawi pia wamejumuishwa katika mchanganyiko huo, lakini Lawi hayumo tena kama mmoja wa wana wa Israeli, kwani Lawi alikua urithi wa Mungu.
Kwa hivyo ni nini kilitokea kwa wana wengine kumi, au makabila, ya mjukuu wa Ibrahimu? Je, wamepotea? Wengi wanafikiri hivyo.
Je, ingewezekana kufuatilia uhamiaji wa wana wengine kumi wa Israeli ili kujua walikokwenda?
Vipi kuhusu unabii? Je, kuna chochote katika Biblia kinachoweza kuonyesha makabila ya kisasa ya Israeli ni akina nani kulingana na utimilifu wa unabii?
